Darasa la mafunzo ya Qur'an Tukufu limeendelea katika Chuo cha Kimataifa cha Al-Mustafa (s) Jijini Dar es Salaam, Tanzania likiongozwa na Al-Haj Sheikh Muhammad Ja'far huku usomaji wa Qur'an ukifanywa na Sheikh Khamis Mpili.

16 Julai 2026 - 17:41

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa (s) tawi la Dar es Salaam, Tanzania, kimeendelea na programu zake za kuwajengea wanafunzi maarifa ya Qur'ani Tukufu kupitia darasa maalumu la mafunzo lililofanyika Alhamisi, tarehe 16 Julai 2026.
 
Darasa hilo liliongozwa na Al-Haj Sheikh Muhammad Ja'far, ambaye aliwasilisha mafunzo yaliyolenga kuimarisha uelewa wa wanafunzi kuhusu usomaji sahihi wa Qur'an Tukufu, Tajwid, pamoja na kutafakari maana za Aya za Qur'an Tukufu.
 
Kabla ya mafunzo hayo, usomaji wa Qur'ani Tukufu uliongozwa na Sheikh Khamis Mpili, ambaye aliwasomea washiriki aya za Qur'ani kwa kufuata kanuni za Tajwid na usomaji sahihi.
 
Uongozi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa (s) unaendelea kuweka mkazo katika malezi ya kielimu na kiroho kwa wanafunzi, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuisoma, kuielewa na kuifuata Qur'ani Tukufu katika maisha yao ya kila siku.
 
Mafunzo hayo ni sehemu ya ratiba endelevu ya chuo inayolenga kuandaa wanazuoni na waalimu wenye elimu madhubuti ya Qur'ani na mafundisho ya Ahlul-Bayt (as), ili waweze kulitumikia Umma wa Kiislamu kwa ufanisi.

Maoni yako

You are replying to: .
captcha